• KARIBU
    IDARA YA UINJILISTI TAG
    "Miaka kumi na tatu ya moto wa uamsho_Tunamtaka BWANA na nguvu zake."
  • Tovuti ya idara ya Uinjilisti
    TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

Kuhusu Idara

Huduma ya Uinjilisti ilianza rasmi Mwaka 1940 kupitia Wazee wetu (Wainjilisti watano); Rev Emmanuel Lazaro, Rev Moses Kulola, Rev Christian Kiwia, Ev Mathias Ng’andu na Rev Daudi Kuselya. Hawa walikuwa Wainjilisti wa mwanzoni kabisa ambao walihubiri kila kona ya Tanzania na kuhakikisha wanapanda makanisa Mwaka 2004, Idara ya Uinjilisti ilianzishwa rasmi katika kanisa la TAG, baada ya pendekezo la kuanzishwa kwake na kupitishwa na Halmashauri Kuu. Pamoja na mikutano Mikubwa ya Injili iliyofanyika huko nyuma, bado hapakuwa na chombo rasmi kitaifa cha kuratibu huduma hizi za Uinjilisti isipokuwa kulikuwa na Kamati tu zilizoundwa kwa kusudi husika la kuandaa mikutano hiyo mpaka mwaka 2004 ambapo Idara ya Uinjilisti Kitaifa ilipoanzishwa rasmi.


DHIMA

Ni kuhakikisha Injili inahubiriwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu, Kwa njia inayoendana na mazingira ili watu wa Tanzania na ulimwenguni kote wapate kusikia habari za Bwana na Mwokozi Yesu Kristo.

KUSUDI

  • Kuhamasisha na kueneza huduma za Uinjilisti kitaifa.
  • Kuleta Uamsho na kutunza utakatifu ili moto wa Uamsho usizimike.
  • Kuibua na kuibua vipawa vya uinjilisti wa ngazi mbalimbali.

MAADILI

  • Uaminifu kwa Biblia.
  • Uadilifu.
  • Wajibu kwa jamii kwa kuonesha taswira ya upendo na haki kwa watu wote.
  • Kuvuna kwa pamoja.
  • Kuvuna Kimkakati.